Thank you for these amazing days at MamboViewPoint! We were immediately stunned by the beauty of MamboViewPoint. The view, the weather, the food, the hospitality, the Hiking, all spectacular!! What an amazing delight to find you at the top of the mountain. We were very happy to stay in one of the most beautiful places of Tanzania.
         
      
MamboViewPoint EcoLodge                                                                      gbflag nl_flag Tz_flagGerman fr_flag
Tuko Tanzania na sehemu kubwa ya mtandao wetu ni Kiingereza ili kuwahudumia watu wengi kimataifa. Tunatumaini mtatuelewa na hamtasita kututembelea.
 Click here for the English website
MamboViewPoint ni hoteli inayohusiana na mazingira ya asili iliyoko Tanzania upande wa Kaskazini mwa  milima ya Usambara.  Magharibi kwenye kijiji cha Mambo, Tarafa ya Mtae* 
 

Karibu hoteli ya MamboViewPoint eco lodge

MV_Poster
Ukiwa unasafiri kutoka Lushoto  kwenye milima  ya Usambara yenye mandhari mbalimbali, njia za asili zinazozunguka milima navijiji vilivyoko juu ya vilima hutategemea  kukuta pepo ndogo kama MVP. Utafurahia mandhari  mbalimbali, mapumziko yako,ama shughuli yeyote itakayokufanya usisahau  safari yako.

 
Mambo
Mambo ni kijiji chenye wastani wa wakazi 5000 wenye kipato chini ya dola moja ya Kimarekani kwa siku.  Maendeleo yanahitajika katika nyanja mbalimbali. MVP inachangia kwa maendeleo ya sehemu husika.
 
ViewPoint
Hoteli ipo kwenye mwinuko  wa meta 1900 juu ya usawa wa bahari mahali ambapo unaweza kufurahia mandhari za milima ya Upare, Mbuga ya Taifa Mkomazi na Mlima Kilimanjaro mrefu kuliko yote Africa. Vilevile  ViePoint inamaanisha mtizamo wa kazi tunazofanya.
  
 
FixHouse
LuxTent
cliffs
ServiceArea
Overlanders
Biking
KidhegeFalls
climbing
 
english
Eco&Details
Eco
Kutokana na mtizamo wa MamboViewPoint, eco inazingatia yafuatayo;
 
. Matumizi ya vitu vya asili vinavyopatikana kwenye mazingira yake.
. Matumizi ya nguvu za umeme  zinazotokana na nguvu za asili kama jua
   na upepo.
. Matumizi madogo ya maji.
. Maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eneo husika.
. Utalii wenye usawa; Utalii wenye kuzingatia mazingira na jamii husika.
 
MamboViewPoint imeorodheshwa kwenye daraja la juu la mahoteli ya aina hiyo na taasisi mbalimbali za kimataifa zinazosimamia mahoteli hayo.
 
Tafadhali bonyeza hapa ili usome sera zetu za mzingira (kiingereza tu)
 
Unakaribishwa kuzisoma!
 
Ushirikiano mpana
 
MamboViewPoint ni kama kiungo kati ya wenye nacho  kwenye nchi zilizoendelea na wenyeji wa milima ya Usambara. Mashariti ya msingi kwa wafadhili si kutoa msaada bali walenge kushirikiana kwa usawa. MVP itasaidia kuandaa aina za miradi, michanganuo, utekelezaji na kusimamia iwe endelevu. Kwenye kipindi cha  utekelezaji, wafadhili wanaweza kufanya kazi za mradi wao wakiwa wanalala kwa raha kwenye hoteli ya MamboViewPoint.  Gharama za ziada za mradi zitapungua, na mfadhili ataona kinachofanyika na matokeo yake.
Mfadhili akiondoka ,MVP itasimamia mradi ili usife uwe endelevu.
Vitu vingi  vidogo vidogo vilivyokamilikavinaweza kuleta maendeleo ya wananchi wa Usambara.   Miradi midogo midogo ya wananchi inaweza kusimamiwa kwa njia hii;kwanyongeza, likizo ya mapumziko ukiwa milima ya Usambara itakuhakikishia uzoefu wa mazingira na utamaduni ambao hutausahau .
Karibu sana!   
 
Marion Neidt, Ndege Chombo, Herman Erdtsieck
MamboViewPoint Map
Mambo * Mambo ni kijiji kilichopo kwenye milima ya Usambara  karibu na Mtae, ambayo hufahamika kwenye vitabu vingi. Usijichanganye na Mombo (watu wengi wameshafanya hivyo) ambao ni mji mdogo  uliyoko njia panda ya Lushoto.
Tuko Tanzania na sehemu kubwa ya mtandao wetu ni Kiingereza ili kuwahudumia watu wengi kimataifa.  Tunatumaini mtatuelewa  na hamtasita kututembelea.
 Click here for the English website
MamboViewPoint  Mambo/Mtae/Lushoto Tanzania                                                                Home